1 Corinthians 7

1Kuhusu mambo mliyoniandikia: Kuna wakati ambapo ni vizuri mwanaume asilale na mke wake. 2Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe.

3Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe. 4Si mke aliye na mamlaka juu ya mwili wake, ni mme. Na vile vile, mme naye hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke anayo.

5Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi. 6Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri. 7Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile.

8Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi. 9Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa heri kwao kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

10Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. “Mke asitengane na mme wake.” 11Lakini kama akijitenga kutoka kwa mmewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mmewe. Na “Mme asimpe talaka mke wake.”

12Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha. 13Kama mwanamke ana mme asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache. 14Kwa mme asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mmewe aaminiye. Vinginevyo watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.

15Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka na aende. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16Unajuaje kama mwanamke, huenda utamwokoa mmeo? Au unajuaje kama mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?

17Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote. 18Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa. 19Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.

20Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini. 21Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hiyo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo. 22Kwa mmoja aliyeitwa na Bwana kama mtumwa ni mtu huru katika Bwana. Kama vile, mmoja aliye huru alipoitwa kuamini ni mtumwa wa Kristo. 23Mmekwisha nunuliwa kwa thamani, hivyo msiwe watumwa wa wanadamu. 24Kaka na dada zangu, katika maisha yoyote kila mmoja wetu tulipoitwa kuamini, tubaki kama vile.

25Sasa, wale wote ambao hawajaoa kamwe, sina amri kutoka kwa Bwana. Lakini nawapa maoni yangu kama nilivyo. Kwa huruma za Bwana, zinazo aminika 26Kwa hiyo, ninafikiri hivyo kwa sababu ya usumbufu, ni vyema mwanaume abaki kama alivyo.

27Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke. 28Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.

29Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana. 30Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote. 31Na wote wanaoshughulika na ulimwengu, wawe kama hawakushughulika nao. Kwa kuwa mitindo ya dunia inafikia mwisho wake.

32Ninataka muwe huru kwa masumbufu yote. Mwanaume asiyeoa anajihusisha na vitu vinavyo mhusu Bwana, namna ya kumpendeza yeye. 33Lakini mwanaume aliyeoa hujihusisha na mambo ya dunia, namna ya kumpendeza mkewe, 34amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.

35Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.

36Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi. 37Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa. 38Hivyo, anayemwoa mwanamwali wake afanya vyema, na yeyote ambaye anachagua kutooa atafanya vyema zaidi.

39Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu. Bado katika maamuzi yangu, atakuwa na furaha zaidi kama akiishi kama alivyo. Na ninafikiri kuwa nami pia nina Roho wa Mungu.

40

Copyright information for SwaULB